How to get Best Church YouTube Channel
You will get the Best Chanel please learn these few steps from
๐@youtubetacticswithmikewing9321
https://youtu.be/MVKQO2NpUZo?si=9t8estqvoqWeOIFm&list=PLB2Se7JSfA-fpipF0z8ehqgg3YdCESVlF&si=cCVwFAWC-7XHPvRQ
Na Mwandishi Wetu,Singida.
WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU NA KAMERA ZENU KWA WELEDI
Waandishi wa Habari Mkoa Singida Wapatiwa Semina Na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Nchini Takukuru Kuelekea Uchaguzi Mkuu Wa Rais , Wabunge na Madiwani Tar 29/10/2025
Akifungua Semina hiyo Mkuu Wa Takukuru Mkoa wa Singida Sosthenes Kibwengo amesema , Waaandishi wa Habari kama mhimili wa nne usio Rasmi ni Wadau mhimu Katika mapambano dhidi ya rushwa kwakuwa ni daraja kati ya wananchi na serikali hivyo wanapotumia kalamu na kamera zao vizuri kuhusu ripoti juu masuala ya rushwa itasaidia kuleta matokeo mazuri.
Kwa mjibu wa Bw. Kibwengo Waandishi wa Habari wanapaswa kufanya Kazi yao Kwa weledi,wakizingatia maadili Yao Bila kujihusisha na rushwa hasa wakati wa Uchaguzi Hali inayopelekea Kuandika na kuripoti Habari Kwa upendeleo kwasababu wamepokea rushwa Kutoka Kwa baadhi ya wagombea au Vyama.
Aidha, Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Singida Ameongeza kuwa Waandishi wa Habari wanaojihusisha na rushwa hawawezi kuieleza Jamii uhalisia wa madhara ya rushwa yatakayotokea baadae kama kutotekelezwa Kwa miradi wanayoahidi baadhi ya wagombea Kwa kuwa walitumia ahadi za uongo baada ya kutoa hongo wanapochaguliwa kipaumbele chao Huwa kurudisha pesa au mali walizotoa kama zawadi za Hila Kwenye kampeni na kushindwa kutatua kero za wananchi.
Hata hivyo Waandishi wa Habari walioshiriki Semina hiyo wamepongeza juhudi za Takukuru mkoa wa Singida Kwa kufanikisha kupeleka watuhumiwa wa rushwa mahakamani na kushinda zaidi ya asilimia sabini ya kesi,Kwa Mwaka 2024, kutoa Semina kama hizi Kwa makundi mbalimbali na kuahidi kushirikiana na Takukuru.
Waandishi wa Habari Mkoa Wa Singida Watahadharishwa Kuhusu Viashiria vya Rushwa Wakati wa Uchaguzi
Na Mwandishi Wetu,Wajefya Radio – SingidaWaandishi wa habari mkoani Singida wametakiwa kuongeza umakini katika majukumu yao hasa nyakati za uchaguzi, kwa kuvitambua mapema viashiria vya rushwa na kuviarifu wananchi ili jamii ijikinge navyo. Wito huo umetolewa leo katika semina ya mafunzo iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ikilenga kuwajengea uwezo wanahabari kuelekea chaguzi zijazo.
Akizungumza katika semina hiyo, Mwezeshaji Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Takukuru mkoa wa Singida, Bwana Benjameni Masyaga, amesema rushwa ya uchaguzi ni moja ya vitendo vinavyohatarisha demokrasia na haki za wananchi. Alisisitiza kuwa waandishi wa habari ni daraja muhimu kati ya jamii na vyombo vya usimamizi wa uchaguzi, hivyo wanapaswa kutumia kalamu zao kulinda uadilifu wa kura ya wananchi.
Kwa mjibu wa Masyaga alivitaja viashiria vitano vinavyoweza kujitokeza nyakati za uchaguzi, ambavyo waandishi wanapaswa kuvifuatilia na kuviripoti kwa ufasaha:
Kugawa fedha au zawadi kwa wapiga kura – Jaribio la kununua kura badala ya kushindana kwa hoja na sera.
Matumizi mabaya ya rasilimali za umma – Kuingiza magari, fedha au majengo ya serikali kwenye kampeni binafsi.
Ahadi za upendeleo binafsi – Kutoa ahadi za ajira, biashara au mikopo kwa lengo la kushawishi kura.
Vitisho kwa wapiga kura – Kuwatisha wapiga kura watakosa ajira au huduma fulani endapo hawatampigia kura mgombea fulani.
Habari za upotoshaji kwenye vyombo vya habari na mitandao – Kutumia taarifa za uongo au propaganda kuchafua wapinzani.
Hata hivyo Bw.Masyaga, Ameongeza kuwa Takukuru hutumia mikakati kadhaa kudhibiti vitendo hivi ikiwemo:
Kutoa elimu ya uadilifu kwa wananchi na vyama vya siasa.
Kufanya ufuatiliaji wa karibu katika maeneo ya kampeni na vituo vya kupigia kura.
Kushirikiana na Jeshi la Polisi ,Tume ya Uchaguzi na Wadau Mbalimbali.
Kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Aisha,Bw.Masyaga alieleza kuwa rushwa ikiachwa, huharibu msingi wa demokrasia na kupelekea kuchaguliwa viongozi kwa misingi ya fedha badala ya sera na uwezo. Matokeo yake ni kushuka kwa imani ya wananchi kwa mchakato wa uchaguzi, kuzorota kwa maendeleo, na kuzuka kwa migawanyiko ya kijamii.
Pamoja na Hayo Zipo Changamoto zinazowakabili Wanahabari katika nafasi yao muhimu kuisaidia Jamii dhidi ya mapambano haya ya Rushwa, Bw.Masyaga alisema bado kuna mianya inayoweza kudhoofisha ufanisi wa waandishi wa habari nyakati za uchaguzi ikiwa ni pamoja na:
Kukosa taarifa za uhakika kuhusu matukio ya rushwa.
Shinikizo kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari wenye maslahi ya kisiasa.
Hali ngumu za kiuchumi zinazoweza kuwafanya baadhi ya waandishi kushawishika kwa hongo.
Hofu ya usalama binafsi au ajira kwa kuripoti habari zinazohusu wagombea wenye nguvu.
Upungufu wa mafunzo ya kitaaluma kuhusu sheria na taratibu za uchaguzi.
Akihitimisha, Masyaga aliwaomba waandishi wa habari mkoani Singida kushirikiana kwa karibu na TAKUKURU, kushikilia maadili ya uandishi, na kuhakikisha wanatoa taarifa kwa usahihi ili kulinda kura na demokrasia ya Tanzania.
Kwa Ujumla Wao,Waandishi Hao Wa Habari Waliahidi Kuitumia Elimu hii Kwa Jamii na Kuhakikisha wanatumia kalamu,na kamera zao Kwa weledi hasa kuwa daraja kati ya Wananchi ,Takukuru na Mamlaka za Serikali hasa nyakati za uchaguzi Kwa kuripoti Kwa Mizania Sawa.
Makala hii endelevu inalenga kuelimisha jamii kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kudhibiti rushwa za uchaguzi. Waandishi wakitimiza wajibu wao, wananchi watapata mwongozo wa kufanya maamuzi kwa uhuru na bila kushawishiwa na fedha au zawadi.
Kutoka Singida, Na Mwandishi Wa Jimbo Eagt Singida Kati.
KANISA LIMETAKIWA KUWA NA UMOJA.
Wito huo umetolewa Leo na Askofu Dr. Daniel Mwangu Wa Eagt Jimbo La Singida Kati wakati akizungumza Kwenye Semina elekezi na wachungaji Katika Kanisa analochunga La EAGT Kibaoni Mjini Singida.
Dr.Mwangu Alisoma Neno La Mungu Kutoka Yoh.17:11-22"Yohana 17:11-22
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja."
Amesema ikiwa Mungu na Utatu mtakatifu wanajali UMOJA je sisi watumishi wake ambao ametuweka kazini mwake,tusishikamane Ili tufanikiwe kulihudumia kundi lake Kwa Umoja ? Alihoji Dr Mwangu.
Aidha ,Askofu Dr.Mwangu ameonya vikali Wachungaji wanaojipna wao wamekamilika na kutojali huduma za wengine Hali inayoleta kutokaribishana Kwenye makanisa wanayochunga jambo linalopelekea kumeguka Kwa Umoja Kati Yao na kusahau wakristo wanapenda Ushrika.
"Wakristo wanapenda Ushrika,unapowatenga kuzuia kuchangamana na wenzako au kukataa kualika Wachungaji wengine watadumaa Hata ukiwalisha nyama Kila Siku watakunai wakati mwingine walishe mlenda watanawiri" Alisisitiza Askofu Dr.Daniel Mwangu.
Kwa Upande wao Wachungaji ambao wanashiriki Semina hii elekezi,
Mch. Eleizeri Muna,Makamu Mkurugenzi Wa Idara ya vijana CGM,Jimbo,,Mch Matayo Manase,Mkurugenzi Wa Bodi ya Waalimi na Wainjilisti TEBE Jimbo wamesema mafundisho haya yamewaimarisha na kuwatia nguvu kushikamana Sana Hasa Kwenye utumishi wao na Kila moja kujali huduma ya mwenzako Kwa kuujenga mwili wa Kristo.Semina Hii ni maandalizi ya kikao Cha pili Cha kikatiba Kesho Cha mwezi wa sita Kwa mjibu wa kalenda ya vikao ya Eagt ambapo Cha kwanza kilifanyika mwezi wa tatu,ambapo Baada ya kikao watahitimisha Kwenda kuungana na wanawake kufunga kongamano lao La Jimbo linaloendelea Katika Kanisa La EAGT Utemini Kwa Askofu wa Kanda John Mwafimbo likihitimishwa Kwa Utaratibu wa Jimbo Hilo wanawake hao kuwategemeza Wachungaji Kwa kuonyesha wanaithamini na kuwapenda Kwa Kazi kubwa wanayoifanya makanisani mwao.
OMBI LA UFADHILI KWA AJILI YA UNUNUZI WA VIFAA VYA RADIO YA MTANDAONI – WAJEFYA RADIO
https://zeno.fm/radio/wajefya-radio/
Ndugu wapendwa katika Bwana,
Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba msaada wa kifedha ili kuwezesha ununuzi wa vifaa Bora Vya kisasa na Vya muhimu kwa ajili ya kuendesha Radio Yangu ya Wajefya Radio, Radio ya Kikristo ya mtandaoni itakayolenga kueneza Injili vijijini na maeneo yasiyofikiwa kwa urahisi na vyombo vingine vya habari.
UMUHIMU WA WAJEFYA RADIO
1.Mimi ni Mchungaji,Nachunga Kanisa Kwa Taalumu ni Mwanahabari,nimejitolea kuanzisha radio Yangu binafsi Ili kupeleka Injili duniani,Kwa kuwasaidia Wahubiri na Waimbaji Vijijini wasikike Duniani.
2.Huduma zao Kwa njia rahisi.
Hakuna malipo kwao wanaotoa huduma za Mahubiri na Nyimbo zao,Mfano ibada,Tamasha,mikutano,Semina,makongamo nk.
2.Mpaka Sasa Radio ipo hewani tangu tar.05/09/2024 Muda wa saa 24/ Siku 7 za wiki.Sikiliza tuu mtandani pale Google,hivi, Wajefya Radio. Na wanaweza save link hiii kwa kubonyeza hapa
https://zeno.fm/radio/wajefya-radio/
2.Ninatumia Vyombo Vidogo,Ambavyo Nina lengo kuongeza hivyo Vya kisasa Kwa Ajili ya ubora wa Matangazo yetu.
3.Ombi hili linalenga Maboresho na baadae Iwe Kwenye Radio Bila bando,Yaani FM itakayopatikana na Kwenye simu ndogo au Radio za kawaida.
Katika maeneo mengi ya vijijini, watu wengi hawana fursa ya kusikia mafundisho sahihi ya Neno la Mungu kwa sababu ya ukosefu wa vyombo vya habari vya Kikristo. Wajefya Radio inalenga:
1. Kufundisha na Kuhamasisha – Kutoa mafundisho ya Biblia, mahubiri, na nyimbo za injili zinazojenga imani.
2. Kufikia Watu Walio Vijijini – Kupitia teknolojia ya mtandao, tunaweza kufanikisha jukumu la Agizo Kuu la Kristo (Mathayo 28:19-20).
3. Kutoa Elimu na Maendeleo – Mbali na mafundisho ya kiroho, radio pia itakuwa jukwaa la kuelimisha kuhusu afya, maendeleo ya jamii, na maadili.
4. Kuwafariji na Kuwaunganisha Waumini – Wale walioko mbali na makanisa au walio na changamoto za kiroho wanaweza kufikiwa kwa njia hii.
VIFAA VINAVYOHITAJIKA NA GHARAMA ZAKE
Ili kuboresha Wajefya Radio ifanye kazi kwa ufanisi, vifaa vifuatavyo vinahitajika:
1. Kompyuta yenye uwezo wa kuendesha programu za radio – TSh 1,500,000 Au kiasi unachoweza Kuchangia.
2. Mikrofoni ya ubora wa juu kwa utangazaji – TSh 500,000 Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda.
3. Madhani (Audio Mixer) kwa uboreshaji wa sauti – TSh 800,000 au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
4. Headphones za studio kwa udhibiti wa sauti – TSh 300,000
Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
5. Internet Router na malipo ya intaneti ya miezi 6 – TSh 900,000
Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
6. Leseni ya Programu ya Utangazaji (Broadcasting Software License) – TSh 600,000
Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
7. Viti na Meza za Studio – TSh 400,000
Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
8. Backup Power Supply (UPS) kwa kuhakikisha matangazo hayakatiki – TSh 700,000
Au kiasi unachoweza Kuchangia Kwa moyo wa Kupenda
Jumla ya Gharama: TSh 5,700,000
OMBI LA MSAADA
Nawaomba ndugu zangu katika Bwana, marafiki, na wadau wote wenye moyo wa kusaidia kueneza Injili, mnisaidie kwa hali na mali ili kufanikisha mradi huu wa Wajefya Radio. Kiasi chochote unachoweza kutoa kitakuwa na thamani kubwa katika kuhakikisha Injili inawafikia watu wengi zaidi, hasa vijijini.
Kwa msaada wowote au mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana nami kupitia:
๐ [Namba ya simu +255698006927,+255622934834]
๐ง [Barua pepe:wajefya.tz@gmail.com.]
Mungu awabariki sana kwa upendo na michango yenu. Tuunganishe sauti zetu kwa Injili!
Kwa Upendo na Shukrani,
[Charles Michael Ntungu]
Mwanzilishi, Wajefya Radio
MOYO WA SHUKRANI UNAPOKEA MEMA
40. Kutoa Shukrani Katika Hali Zote
Jinsi ya Kutumia:
Kuwa na moyo wa kushukuru hata unapokutana na changamoto. Tambua kwamba kila jambo linafanyika kwa kusudi la Mungu.
Mfano:
Paulo aliandika, "Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu katika Kristo Yesu." (1 Wathesalonike 5:18)
Matokeo:
Shukrani inaleta muujiza, furaha, amani, na kibali cha Mungu, hata wakati wa majaribu.
Mwandishi wa Kitabu:
Paulo (Kitabu cha 1 Wathesalonike)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Paulo alihimiza waumini kuwa na moyo wa kushukuru, hata walipokumbana na mateso.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa shukrani kunaweza kupelekea huzuni, kulalamika, na kutokuwa na furaha maishani.
---
41. Kuwa na Moyo wa Kujifunza
Jinsi ya Kutumia:
Jifunze kutokana na uzoefu wako, mafundisho ya Biblia, na watu walio na hekima.
Mfano:
Sulemani alisema, "Mwenye hekima atasikia na kuongeza maarifa." (Mithali 1:5)
Matokeo:
Mwaminifu hupata hekima zaidi na uelewa wa kiroho, akifanya maamuzi bora zaidi.
Mwandishi wa Kitabu:
Sulemani (Kitabu cha Mithali)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kujifunza ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Sulemani aliandika Mithali ili kuwasaidia watu kuelewa hekima ya Mungu.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa moyo wa kujifunza husababisha kukwama kiroho na kutoendelea mbele katika maisha.
---
42. Kukiri Dhambi na Kutubu
Jinsi ya Kutumia:
Kubali makosa yako mbele za Mungu, omba msamaha, na ugeuke kutoka njia zako mbaya.
Mfano:
Daudi alisema, "Nimekukosea Wewe tu, Ee Mungu." (Zaburi 51:4)
Matokeo:
Mungu husamehe, kutakasa, na kurejesha mwamini kwenye ushirika wake.
Mwandishi wa Kitabu:
Daudi (Kitabu cha Zaburi)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kukubali unakosea ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Baada ya dhambi yake na Bathsheba, Daudi alitubu kwa dhati na Mungu akamsamehe.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Dhambi isiyokiriwa husababisha huzuni, kushindwa kiroho, na kutengana na Mungu.
---
43. Kufuata Maongozi ya Mungu
Jinsi ya Kutumia:
Soma Neno la Mungu na uombe mwongozo wa Roho Mtakatifu kabla ya kufanya maamuzi yoyote.
Mfano:
Musa aliwaongoza Waisraeli jangwani kwa kufuata maelekezo ya Mungu kupitia nguzo ya wingu na moto. (Kutoka 13:21-22)
Matokeo:
Mungu anatoa mwongozo wa wazi, na mwamini anapata matokeo mazuri.
Mwandishi wa Kitabu:
Musa (Kitabu cha Kutoka)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru Na kufuata uongozi ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Mungu aliwaongoza Waisraeli kutoka utumwani Misri hadi Nchi ya Ahadi.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa kufuata mwongozo wa Mungu kunaweza kusababisha kupotea na kushindwa kufanikisha malengo ya kiroho.
---
44. Kuwa na Moyo wa Unyenyekevu
Jinsi ya Kutumia:
Epuka kiburi na jiweke chini mbele za Mungu na watu.
Mfano:
Yesu alisema, "Kila ajikwezaye atashushwa, na kila ajishushaye atainuliwa." (Luka 14:11)
Matokeo:
Mungu humuinua mwaminifu anayejishusha na kumtegemea.
Mwandishi wa Kitabu:
Luka (Kitabu cha Luka)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kuwa mnyenyekevu ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Yesu alihimiza watu kuwa wanyenyekevu mbele za Mungu na wanadamu.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kiburi huleta kushushwa na hukumu kutoka kwa Mungu.
---
45. Kushikilia Ahadi za Mungu
Jinsi ya Kutumia:
Soma na ukumbuke ahadi za Mungu zilizopo kwenye Biblia. Tumia ahadi hizo katika maombi yako.
Mfano:
Mungu alimwambia Yoshua, "Sitakuacha wala sitakupungukia." (Yoshua 1:5)
Matokeo:
Mwamini huimarishwa, kutia moyo, na kupata matokeo ya kiroho kupitia ahadi hizo.
Mwandishi wa Kitabu:
Yoshua (Kitabu cha Yoshua)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kushika Hadi za Mungu ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Yoshua alipokea ahadi za Mungu alipokuwa anaongoza Waisraeli.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa kushikilia ahadi za Mungu kunaweza kupelekea hofu na ukosefu wa matumaini.
---
46. Kushinda Kwa Ushuhuda
Jinsi ya Kutumia:
Shiriki matendo makuu ambayo Mungu amefanya maishani mwako ili kuwajenga na kuwahimiza wengine.
Mfano:
Waebrania 12:1 inasema, "Tumezungukwa na wingu kubwa la mashahidi."
Matokeo:
Ushuhuda wako huwasaidia watu kuamini na kumtumaini Mungu zaidi.
Mwandishi wa Kitabu:
Mwandishi wa Waebrania
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kuwashuhudia wengine ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Ushuhuda wa watu wa imani kama Ibrahimu ulitumika kuimarisha waumini wa wakati huo.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa kushuhudia hupelekea kupoteza nafasi za kuleta wokovu na kujenga imani za wengine.
---
47. Kukubali Mafunzo na Nidhamu ya Mungu
Jinsi ya Kutumia:
Chukua mafunzo ya Mungu kwa moyo wa shukrani hata kama ni magumu.
Mfano:
Waebrania 12:6 inasema, "Bwana huwakemea wale awapendao."
Matokeo:
Nidhamu ya Mungu huleta ukomavu wa kiroho na baraka zaidi.
Mwandishi wa Kitabu:
Mwandishi wa Waebrania
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kukubali Maonyo ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Mungu aliwafundisha Waisraeli katika safari yao ya jangwani.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukataa nidhamu ya Mungu huleta matatizo makubwa na kuharibika kwa maisha ya kiroho.
---
48. Kumtumaini Mungu kwa Ukombozi wa Kipekee
Jinsi ya Kutumia:
Mwamini Mungu kwamba anaweza kukuokoa katika hali zisizowezekana.
Mfano:
Mungu aliwatoa Danieli na wenzake kutoka tanuru la moto. (Danieli 3:24-25)
Matokeo:
Mungu hutukuzwa na mwamini huokolewa kutoka hatarini.
Mwandishi wa Kitabu:
Danieli (Kitabu cha Danieli)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kumtumaini Mungu ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Mungu aliwalinda Shadraka, Meshaki, na Abednego katika tanuru ya moto.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa kumtumaini Mungu kunaweza kusababisha kushindwa na kupoteza ushindi.
---
49. Kutegemea Neema ya Mungu
Jinsi ya Kutumia:
Mtegemee Mungu kwa kila jambo. Tambua kuwa nguvu zako hazitoshi, bali neema yake inakutosha.
Mfano:
Paulo alisema, "Neema yangu yakutosha." (2 Wakorintho 12:9)
Matokeo:
Mwaminifu hupata nguvu hata katika udhaifu na changamoto.
Mwandishi wa Kitabu:
Paulo (Kitabu cha 2 Wakorintho)
Tukio Liliotokea:Angalia na Nyakati unazopitia,Waweza Kushukuru na kuwa mwaminifu ukutane na Muujiza Wako? Anza sasa
Paulo alipata nguvu ya kuendelea licha ya changamoto za kiroho na kimwili.
Madhara Iwapo Haitatumika:
Kukosa neema ya Mungu hupelekea mzigo mkubwa na kushindwa kufanikisha mambo.
---
50. Kuwa na Moyo wa Kumshukuru Mungu Kwa Wokovu
Jinsi ya Kutumia:
Sikuzote mshukuru Mungu kwa wokovu ulioupokea kupitia Yesu Kristo.
,,,, Itaendeleaaa , toa maoni yako