Na Mwandishi Wetu,Singida.
WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU NA KAMERA ZENU KWA WELEDI
Waandishi wa Habari Mkoa Singida Wapatiwa Semina Na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Nchini Takukuru Kuelekea Uchaguzi Mkuu Wa Rais , Wabunge na Madiwani Tar 29/10/2025
Akifungua Semina hiyo Mkuu Wa Takukuru Mkoa wa Singida Sosthenes Kibwengo amesema , Waaandishi wa Habari kama mhimili wa nne usio Rasmi ni Wadau mhimu Katika mapambano dhidi ya rushwa kwakuwa ni daraja kati ya wananchi na serikali hivyo wanapotumia kalamu na kamera zao vizuri kuhusu ripoti juu masuala ya rushwa itasaidia kuleta matokeo mazuri.
Kwa mjibu wa Bw. Kibwengo Waandishi wa Habari wanapaswa kufanya Kazi yao Kwa weledi,wakizingatia maadili Yao Bila kujihusisha na rushwa hasa wakati wa Uchaguzi Hali inayopelekea Kuandika na kuripoti Habari Kwa upendeleo kwasababu wamepokea rushwa Kutoka Kwa baadhi ya wagombea au Vyama.
Aidha, Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Singida Ameongeza kuwa Waandishi wa Habari wanaojihusisha na rushwa hawawezi kuieleza Jamii uhalisia wa madhara ya rushwa yatakayotokea baadae kama kutotekelezwa Kwa miradi wanayoahidi baadhi ya wagombea Kwa kuwa walitumia ahadi za uongo baada ya kutoa hongo wanapochaguliwa kipaumbele chao Huwa kurudisha pesa au mali walizotoa kama zawadi za Hila Kwenye kampeni na kushindwa kutatua kero za wananchi.
Hata hivyo Waandishi wa Habari walioshiriki Semina hiyo wamepongeza juhudi za Takukuru mkoa wa Singida Kwa kufanikisha kupeleka watuhumiwa wa rushwa mahakamani na kushinda zaidi ya asilimia sabini ya kesi,Kwa Mwaka 2024, kutoa Semina kama hizi Kwa makundi mbalimbali na kuahidi kushirikiana na Takukuru.
0 comments: