Kutoka Singida, Na Mwandishi Wa Jimbo Eagt Singida Kati.
KANISA LIMETAKIWA KUWA NA UMOJA.
Kanisa La Tanzania limetakiwa kuwa na umoja nyakati zote Ili kuwa na nguvu Hasa linapopitia changamoto za ndani au Kutoka nje kama mwili wa Kristo.
Wito huo umetolewa Leo na Askofu Dr. Daniel Mwangu Wa Eagt Jimbo La Singida Kati wakati akizungumza Kwenye Semina elekezi na wachungaji Katika Kanisa analochunga La EAGT Kibaoni Mjini Singida.
Dr.Mwangu Alisoma Neno La Mungu Kutoka Yoh.17:11-22"Yohana 17:11-22
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja."
Amesema ikiwa Mungu na Utatu mtakatifu wanajali UMOJA je sisi watumishi wake ambao ametuweka kazini mwake,tusishikamane Ili tufanikiwe kulihudumia kundi lake Kwa Umoja ? Alihoji Dr Mwangu.
Aidha ,Askofu Dr.Mwangu ameonya vikali Wachungaji wanaojipna wao wamekamilika na kutojali huduma za wengine Hali inayoleta kutokaribishana Kwenye makanisa wanayochunga jambo linalopelekea kumeguka Kwa Umoja Kati Yao na kusahau wakristo wanapenda Ushrika.
"Wakristo wanapenda Ushrika,unapowatenga kuzuia kuchangamana na wenzako au kukataa kualika Wachungaji wengine watadumaa Hata ukiwalisha nyama Kila Siku watakunai wakati mwingine walishe mlenda watanawiri" Alisisitiza Askofu Dr.Daniel Mwangu.
Kwa Upande wao Wachungaji ambao wanashiriki Semina hii elekezi,
Mch. Eleizeri Muna,Makamu Mkurugenzi Wa Idara ya vijana CGM,Jimbo,,Mch Matayo Manase,Mkurugenzi Wa Bodi ya Waalimi na Wainjilisti TEBE Jimbo wamesema mafundisho haya yamewaimarisha na kuwatia nguvu kushikamana Sana Hasa Kwenye utumishi wao na Kila moja kujali huduma ya mwenzako Kwa kuujenga mwili wa Kristo.Semina Hii ni maandalizi ya kikao Cha pili Cha kikatiba Kesho Cha mwezi wa sita Kwa mjibu wa kalenda ya vikao ya Eagt ambapo Cha kwanza kilifanyika mwezi wa tatu,ambapo Baada ya kikao watahitimisha Kwenda kuungana na wanawake kufunga kongamano lao La Jimbo linaloendelea Katika Kanisa La EAGT Utemini Kwa Askofu wa Kanda John Mwafimbo likihitimishwa Kwa Utaratibu wa Jimbo Hilo wanawake hao kuwategemeza Wachungaji Kwa kuonyesha wanaithamini na kuwapenda Kwa Kazi kubwa wanayoifanya makanisani mwao.